Skip to main content

Na Mashabiki Yanga Mke Wa Carlinhos Adatishwa Na Mashabiki Yanga

 

 
CCCO Vanessa ambaye ni mke wa kiungo mpya wa Yanga, Carlinhos, raia wa Angola, amekuwa akionyesha mahaba yake waziwazi kwa staa huyo kwenye mitandao ya


Lakini juzi alionekana kukunwa na mashabiki wa Yanga kwa jinsi walivyompokea mumewe wakati akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea kwao Angola.

Vanessa alitupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikionyesha jinsi Carlinhos alivyopokewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga, kisha akaandika maneno haya:“Mpenzi wangu…tumshukuru Mungu kwa namna gani? Kwa baraka hiyo, nina furaha hukuacha kujiamini hata kila mmoja alipokoma kukuamini.

Ni Mungu pekee ndiye anayejua nyakati za usiku tulizotumia kwenye maombi.

“Siku zote nilikuambia wakati wako utafika, kipaji, unyenyekevu siku zote zinaendelea kuwa nawe. Ni Baba tu wa mbinguni anayeweza kufanya hayo.

Tunafurahi kujua kwamba umepokewa vizuri katika namna hii kwenye nchi ambayo haijulikani kabisa kwetu.“Mungu aendelee kuwa pamoja nawe, atembee nawe, usimsahau Mungu mpenzi…nakutakia mafanikio endelevu katika hatua hiyo mpya. Fanya kile unachojua kukifanya kwa ubora; KUCHEZA MPIRA.” Wapendanao hao wawili wana watoto watatu.


Comments

Popular posts from this blog

UMUHIMU WA KUFANYA SERVICE OIL KWENYE GARI LAKO

  Kufanya **ervice oil* kwenye gari ni muhimu sana kwa utunzaji na ufanisi wa injini. Hapa kuna sababu kuu za kufanya huduma hii mara kwa mara:    1.Kulinda na Kudumisha Injini - Mafuta ya injini husaidia kulainisha sehemu za injini ili zisichakazane haraka kutokana na msuguano.   - Huondoa uchafu na masalia yanayoweza kuzuia utendaji mzuri wa injini.   2. Kuboresha Utendaji wa Gari - Injini inayopata huduma ya mara kwa mara hufanya kazi kwa ufanisi zaidi.   - Inapunguza msuguano wa sehemu za ndani ya injini, hivyo kuongeza nguvu na utendaji wake.   3.Kuongeza Uhai wa Injini - Mafuta machafu yanaweza kusababisha uchakavu wa injini haraka.   - Kubadilisha mafuta mara kwa mara husaidia injini kudumu kwa muda mrefu bila matatizo makubwa.   4.Kupunguza Matumizi ya Mafuta (Fuel Consumption) - Injini safi na yenye mafuta mazuri hufanya kazi vizuri bila kutumia mafuta mengi.   - Mafuta mabovu au machafu y...

Mariah Carey Apata Pigo Kubwa: Mama na Dada Yake Wafariki Katika Siku Moja

 Mariah Carey ni mmoja wa wasanii wenye vipaji vya kipekee na wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki duniani. Amejulikana kwa sauti yake yenye upana wa oktava tano, uwezo wa kutumia miondoko ya melisma, na matumizi ya kipekee ya "whistle register". Katika mwaka wa 2023, aliorodheshwa kama msanii wa tano bora wa wakati wote na jarida la Rolling Stone. citeturn0search12 Maisha ya Awali na Mwanzo wa Muziki Mariah alizaliwa tarehe 27 Machi 1969 huko Huntington, New York. Alikuwa mtoto wa tatu wa Alfred Roy Carey, mhandisi mwenye asili ya Kiafrika na Kivenezuela, na Patricia Hickey, mwalimu wa muziki na mwimbaji wa opera mwenye asili ya Kiayalandi. Baada ya wazazi wake kutalikiana mwaka 1973, Mariah alikulia na mama yake, ambaye aligundua kipaji chake cha muziki akiwa na umri mdogo. Alianza kuandika nyimbo na kufanya maonyesho akiwa shule ya upili, na baada ya kuhitimu, alihamia Manhattan kufuata ndoto yake ya muziki. citeturn0search15 Mafanikio yake yalianza alipo...

S2Kizzy: Kutoka Mbeya Mpaka Pluto Republic – Safari ya Mfalme wa Beats za Bongo

  Maisha ya S2Kizzy: Safari ya Mtayarishaji Bora wa Muziki Tanzania Salmin Kasimu Maengo, anayejulikana zaidi kwa jina la kisanii S2Kizzy au Zombie, alizaliwa tarehe 9 Mei 1996 huko Mbeya, Tanzania. Baada ya mama yake kufariki akiwa na umri wa miaka mitatu, alilelewa na shangazi yake. Baba yake aliondoka na kuoa tena, hali iliyomfanya S2Kizzy kukua katika mazingira ya changamoto. Alianza kujifunza muziki akiwa mdogo, akicheza ngoma shuleni. Wakati wa masomo yake katika shule ya sekondari ya bweni ya Kwiro Boys High School huko Morogoro, alijifunza kutengeneza muziki kwa kutumia kompyuta ya mwalimu wake. Alitumia likizo zake kubaki shuleni, akidai kuwa alikuwa amepewa adhabu, ili aweze kuendelea na mafunzo yake ya muziki. Kipaji na Mafanikio S2Kizzy alijizolea umaarufu mkubwa kwa kutayarisha nyimbo maarufu kama "Tetema" na "Amaboko" za Rayvanny akimshirikisha Diamond Platnumz. Amefanya kazi na wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz, Rayvanny, Vanessa Mdee, Bill Nass, ...