Nyota wa muziki toka Nigeria, David Adedeji Adeleke 'Davido' amerodheshwa kuwa miongoni mwa washiriki wa filamu ya "Coming To America" sehemu ya Pili ambayo inatarajiwa kutoka rasmi Disemba 18, 2020.
Coming to America ni filamu maarufu ya ucheshi ambayo sehemu ya kwanza ilitoka mwaka 1988 ikiwa na mwigizaji mkongwe Eddie Murphy.
Nafasi hii kwa staa huyo inamfanya kuwa miongoni mwa mastaa wapya ndani ya filamu hiyo watakaoonekana sehemu ya pili, wengine ni Tracy Morgan, Wesley Snipes, Jermaine Fowler, Leslie Jones, Rotimi, Rick Ross pamoja na Michael Blackson.
Comments
Post a Comment