Skip to main content

Afya Ya Wema Sepetu Wingu Latanda September 11, 2020




Staa wa filamu Bongo Muvi, Wema Sepetu.

NINI kimemkondesha msanii Wema Sepetu? Majibu ni mengi kuzidi swali lenyewe kiasi cha kufanya afya yake kuleta wingu zito miongoni mwa mashabiki wake.


Imeelezwa mara kadhaa kuwa, kukonda kwa msanii huyo aliyepata kuwa Miss Tanzania 2006, kumetokana na upasuaji wa kukatwa utumbo aliofayiwa nchini India wenye lengo la kumfanya apungue baada ya kunenepeana.



Hata hivyo, mwenyewe amekuwa akisema “hali hiyo inatokana na msongo wa mawazo unaotokana na mambo ya kimapenzi.


”Ingawa wembamba siyo ugonjwa lakini histori ya “kufungashia” aliyonayo msanii huyo huenda ndiyo inayomtesa, kwani wengi wamekuwa wakimtazama kwa mtazamo hasi.


“Jamani hivi huyu dada ana tatizo gani, webamba huu siyo bure, kimbunga kikipita si kinaondoka naye,” aliandika mtu mmoja kwenye mtandao wa Instagram ambako picha ya Wema ‘aliyekonda’ ilipostiwa.



Hata hivyo, msanii huyo amekua akikerwa na kauli za “umekonda” ambapo mara kadhaa amekuwa akiwajibu vibaya mashabiki wake wanaomsema hivyo.


“Naugua virusi vya HIV ndiyo maana nimepungua kilo,” Wema alimjibu hivyo shabiki yake aliyekomenti kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya msanii huyo kuposti picha, Februari mwaka huu, akiwa na dada yake na shabiki kumwambia kuwa “amekonda.



”Katika kuonesha kwamba watu wanampenda “Wema bonge nyanya” wengi wao wamekuwa wakitafsiri kukonda kwake na tatizo la kiafya kiasi cha kutamani arudie mwili wake wa zamani.


“Wema wa zamani alikuwa akipita mtaani watu wanajipanga foleni kumshangaa jinsi alivyokuwa kafungashia.“Leo wakitoka watamshangaa jinsi alivyokonda na kubaki mifupa,” aliandika mwingine kwenye mtandao wa kijamii.



Februari 4, mwaka jana kupitia mahojiano maalumu na mwandishi wetu kuhusu kukonda kwake msanii huyo alisema:“Yaani hujui tu ninavyoufurahia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa siyo mzito tena, navaa nguo ambazo nataka na ninapendeza zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwa kifupi najipenda hivi nilivyo.”Ingawa mrembo huyo anasema anajipenda jinsi alivyo, wanaompenda zaidi bado wanatatizika na kukonda kwake.


Mara kadhaa kumekuwa kukienezwa taarifa zisizokuwa na ukweli kwamba Wema amekuwa akidondoka na kupoteza fahamu huku kukonda kwake kukihusishwa na hali hiyo.Hata hivyo, mwenyewe amekuwa akikana kutokewa na hali hiyo na kusisitiza kwamba yuko sawa kiafya.



Daktari Fredrik Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili amewahi kuwaonya watu wanaotumia dawa kwa lengo la kupunguza miili yao na kuwataka wawe makini.


“Baadhi ya watu wanatumia dawa za kupunguza uzito bila kupata ushauri wa wataalamu, pia sina uhakika sana ila dawa nyingi za kupunguza uzito nchini kwetu hazijapata vibali, nyingi ni dawa za mtaani ambapo kiukweli zingine si dawa za uhakika au zinatumia njia ambazo si sahihi.


“Kuna watu wanazitumia na kuona kuwa wanapungua mwili kumbe wana sinyaa na hivyo kuwa katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya,” Dokta Mashili anasema.


Uchunguzi unaonesha kuwa Wema amekuwa akizidi kupungua kadiri siku zinavyozidi kwenda, jambo ambalo linawafanya watu wapate hofu juu ya afya yake.



Agosti 2, mwaka jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema aliandika hivi: “Daaaaah kutokana na Comments za watu wengi, inaonekana wengi wanasema ninenepe tena jamani… Ila si ni nyinyi mlonisema nimekuwa Boooooongeee na ilibidi nipungue…


Leo nimeamini Binaadam hamna jema.“Anyways, I will soon Share The Secret to my weight loss na Msijali nitajitahidi kula kula kidogo ili niongezeke hata kidogo tu… Just so you know nilikuwa nina 109kgs na sasa nina 68kgs.”Hayo ni maneno ya Wema mwaka jana lakini kwa kipimo cha macho kisichokuwa na uhakika huwenda msanii huyo amepungua zaidi ya alivyokuwa wakati anaandika komenti hiyo.Kipi cha kushika kuhusu kukonda kwa Wema, linabaki kuwa wingu hakuna wa kulishika zaidi ya kulitazama jinsi linavyochukuliwa na upepo

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya Arsène Wengers

  Arsène Wenger ni mmoja wa makocha mashuhuri zaidi katika historia ya soka, hasa kwa mchango wake katika klabu ya Arsenal ya Uingereza. Alizaliwa tarehe 22 Oktoba 1949, huko Strasbourg, Ufaransa. Kazi yake ya ukocha ilianza baada ya kupata shahada ya uchumi na kucheza soka kama mchezaji wa kiwango cha chini. Baada ya kustaafu kutoka kucheza, Wenger alianza kazi yake kama kocha kwa mara ya kwanza huko AS Nancy-Lorraine mwaka 1984. Alifanya kazi kwa muda mfupi huko kabla ya kuhamia AS Monaco mwaka 1987. Akiwa Monaco, aliwasaidia kushinda Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mwaka 1988, jambo lililomfanya apate umaarufu kama kocha mwenye uwezo mkubwa wa kukuza vipaji. Hata hivyo, baada ya miaka kadhaa Monaco, Wenger aliachishwa kazi mwaka 1994 kutokana na matokeo mabaya, na akahamia klabu ya Grampus Eight huko Japan mwaka 1995, ambapo alipata mafanikio ya haraka kwa kushinda Kombe la Mfalme. Mwaka 1996, Wenger aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Arsenal, na hapo ndipo alipoanza kuwa maarufu zaid...

UMUHIMU WA KUFANYA SERVICE OIL KWENYE GARI LAKO

  Kufanya **ervice oil* kwenye gari ni muhimu sana kwa utunzaji na ufanisi wa injini. Hapa kuna sababu kuu za kufanya huduma hii mara kwa mara:    1.Kulinda na Kudumisha Injini - Mafuta ya injini husaidia kulainisha sehemu za injini ili zisichakazane haraka kutokana na msuguano.   - Huondoa uchafu na masalia yanayoweza kuzuia utendaji mzuri wa injini.   2. Kuboresha Utendaji wa Gari - Injini inayopata huduma ya mara kwa mara hufanya kazi kwa ufanisi zaidi.   - Inapunguza msuguano wa sehemu za ndani ya injini, hivyo kuongeza nguvu na utendaji wake.   3.Kuongeza Uhai wa Injini - Mafuta machafu yanaweza kusababisha uchakavu wa injini haraka.   - Kubadilisha mafuta mara kwa mara husaidia injini kudumu kwa muda mrefu bila matatizo makubwa.   4.Kupunguza Matumizi ya Mafuta (Fuel Consumption) - Injini safi na yenye mafuta mazuri hufanya kazi vizuri bila kutumia mafuta mengi.   - Mafuta mabovu au machafu y...

KESI INAYO MSUMBUWA MSANII SEAN COMBS MAARU KWA JINA P.DIDDY

 Sean Combs Anayejulikana zaidi kwa jina la kisanii P. Diddy ni mojawapo ya kesi zinazoibua mjadala mkubwa katika ulimwengu wa burudani na sheria. Katika miaka ya hivi karibuni, P. Diddy amekuwa akihusishwa na mashtaka kadhaa yanayohusiana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, matumizi mabaya ya madaraka, na unyanyasaji wa kimwili. Moja ya kesi za hivi karibuni ambazo zimechukua nafasi kubwa ni ile inayomuhusisha msanii wa kike aliyewahi kuwa chini ya lebo ya Bad Boy Records, inayomilikiwa na Diddy. Msanii huyo alitoa tuhuma nzito dhidi ya P. Diddy, akidai kuwa alinyanyaswa kingono na kihisia wakati wa uhusiano wao wa kikazi. Msanii huyo anadai kwamba P. Diddy alitumia nguvu na vitisho ili kudhibiti maisha yake binafsi na ya kitaaluma. Kesi hii imevuta hisia na tahadhari kubwa kutoka kwa mashabiki, vyombo vya habari, na wanasheria. Wengi wameibua maswali kuhusu utamaduni wa unyanyasaji na ukatili katika tasnia ya muziki, hasa miongoni mwa watu wenye nguvu kama P. Diddy. Katika ut...