Skip to main content

Posts

Showing posts from 2020

Maneno ya Petit Man kwa Country boy baada ya kuondoka kwake na kusainiwa na Harmonize Konde Gang

  Mdau wa muziki wa mfanyabishara Petit Man ametoa amoni yake kuhusu Rapper Country boy kusainiwa na lebo ya Konde Gang iliyopo chini ya Harmonize. Patit amewajibu watu wanaodai kuwa Country boy ni msanii mkubwa na hakupaswa kusainiwa na Harmonize bora angeanzia lebo yake. Patit pia ameongeza kuwa katika wasanii wote wa Bongo Fleva ambao amewahi kuwa nao karibu hakuna msanii wmenye nidhamu kama Country boy pamoja an Younglunya.

Na Mashabiki Yanga Mke Wa Carlinhos Adatishwa Na Mashabiki Yanga

    CCCO Vanessa ambaye ni mke wa kiungo mpya wa Yanga, Carlinhos, raia wa Angola, amekuwa akionyesha mahaba yake waziwazi kwa staa huyo kwenye mitandao ya Lakini juzi alionekana kukunwa na mashabiki wa Yanga kwa jinsi walivyompokea mumewe wakati akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea kwao Angola. Vanessa alitupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikionyesha jinsi Carlinhos alivyopokewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga, kisha akaandika maneno haya:“Mpenzi wangu…tumshukuru Mungu kwa namna gani? Kwa baraka hiyo, nina furaha hukuacha kujiamini hata kila mmoja alipokoma kukuamini. Ni Mungu pekee ndiye anayejua nyakati za usiku tulizotumia kwenye maombi. “Siku zote nilikuambia wakati wako utafika, kipaji, unyenyekevu siku zote zinaendelea kuwa nawe. Ni Baba tu wa mbinguni anayeweza kufanya hayo. Tunafurahi kujua kwamba umepokewa vizuri katika namna hii kwenye nchi ambayo haijulikani kabisa kwetu.“Mungu aendelee kuwa pamoja nawe, atembee n...

Davido ndani ya filamu ya

  Nyota wa muziki toka Nigeria, David Adedeji Adeleke 'Davido' amerodheshwa kuwa miongoni mwa washiriki wa filamu ya "Coming To America" sehemu ya Pili ambayo inatarajiwa kutoka rasmi Disemba 18, 2020. Coming to America ni filamu maarufu ya ucheshi ambayo sehemu ya kwanza ilitoka mwaka 1988 ikiwa na mwigizaji mkongwe Eddie Murphy. Nafasi hii kwa staa huyo inamfanya kuwa miongoni mwa mastaa wapya ndani ya filamu hiyo watakaoonekana sehemu ya pili, wengine ni Tracy Morgan, Wesley Snipes, Jermaine Fowler, Leslie Jones, Rotimi, Rick Ross pamoja na Michael Blackson.

Diamond atia neno mara ya kwanza tangu Wasafi FM ifungiwe na TCRA, wafanyakazi kufungasha virago

Diamond atia neno mara ya kwanza tangu Wasafi FM ifungiwe na TCRA, wafanyakazi kufungasha virago udakuspecially.comSep 14, 2020 D iamond atia neno mara ya kwanza tangu Wasafi FM ifungiwe na TCRA, wafanyakazi kufungasha virago September 13, 2020 Diamond Platnumz atia neno mara ya kwanza tangu Wasafi FM ifungiwe na TCRA Kutokana na Kukiuka Maadali ya Utangazaji, wafanyakazi Wafunguka kufungasha virago

Zari Yamfika Mazito Kutoka Kwa Wananzengo

Mwanamama mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa muziki barani afrika, Nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’ yamemfika mazito kutoka kwa wananzengo, kisa kikiwa ni mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto. Chanzo cha yote ni baada ya Mobeto kumposti Diamond au Mondi ambaye naye pia ni mzazi mwenzake kwenye ukurasa wake wa Instagram. Zari amejikuta akishambuliwa kutokana na kile alichokiposti Mobeto kuhusu Mondi kuwepo nyumbani kwake huku akiwa na mtoto wao, Abdul Nasibu ‘Dyllan’. Mobeto aliposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha baba na mwana wakiwa na furaha kwelikweli.Baada ya kuposti video hiyo, mashabiki waliibuka na kuanza kumshambulia Zari kuwa watu na baba zao yeye yuko wapi?“Watu na baba zao, wale Wasauzi (Zari na wanaye Tiffah na Nillan) wako wapi, mbona Simba (Mondi) haendi huko?’’ Aliandika shabiki mmoja. Hata hivyo, baadhi ya maoni hayaandikiki kwa kuwa yanamuondolea Zari utu, lakini wapo walioonesha kumtetea mwanamam...

Country Boy afunguka haya baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa gari na Harmonize

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye ni Rapper Country Boy ameongea kwa mara ya kwanza akiwa chini ya lebo ya Konde Gang iliyopo chini ya Harmonize mara tu baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa gari lake mpya.

Afya Ya Wema Sepetu Wingu Latanda September 11, 2020

Staa wa filamu Bongo Muvi, Wema Sepetu. NINI kimemkondesha msanii Wema Sepetu? Majibu ni mengi kuzidi swali lenyewe kiasi cha kufanya afya yake kuleta wingu zito miongoni mwa mashabiki wake. Imeelezwa mara kadhaa kuwa, kukonda kwa msanii huyo aliyepata kuwa Miss Tanzania 2006, kumetokana na upasuaji wa kukatwa utumbo aliofayiwa nchini India wenye lengo la kumfanya apungue baada ya kunenepeana. Hata hivyo, mwenyewe amekuwa akisema “hali hiyo inatokana na msongo wa mawazo unaotokana na mambo ya kimapenzi. ”Ingawa wembamba siyo ugonjwa lakini histori ya “kufungashia” aliyonayo msanii huyo huenda ndiyo inayomtesa, kwani wengi wamekuwa wakimtazama kwa mtazamo hasi. “Jamani hivi huyu dada ana tatizo gani, webamba huu siyo bure, kimbunga kikipita si kinaondoka naye,” aliandika mtu mmoja kwenye mtandao wa Instagram ambako picha ya Wema ‘aliyekonda’ ilipostiwa. Hata hivyo, msanii huyo amekua akikerwa na kauli za “umekonda” ambapo mara kadhaa amekuwa akiwajibu vibaya mashabiki wake wanaomsema hi...

Ndoa ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Na Zuhura Othuman ‘Zuchu’, October 2

  LICHA ya mwenyewe kutoanika kinaga ubaga kuhusu mkewe mtarajiwa, lakini kuna mambo yameanikwa ambayo yanashangaza endapo staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ataamua kuingia kwenye ndoa na mtoto mzuri Zuhura Othuman ‘Zuchu’, IJUMAA WIKIENDA linakupa habari mpya inayowahusu! MNAJIMU AFUNGUKA Hiyo imetokana na gazeti hili kuzungumza na Mnajimu Maalim Hassan Yahya Hussein, ambaye pamoja na mambo mengine, ameeleza maajabu ya nyota za wawili hao na jinsi ambavyo zinashabihiana na kwamba, watafanya makubwa wakiwa pamoja. “Zuchu na Mondi nyota zao zinaendana, kwa sababu ni mizani na ng’e, maana ni nyota ambazo ziko jirani, kama wataamua kuwa pamoja na kuoana, watakaa vizuri. “Katika mwezi wa kumi mwishoni, inaanza nyota ya ng’e, hivyo Diamond kazaliwa Oktoba nyota yake ni mizani na Zuchu kazaliwa Novemba nyota yake ni ng’e, ndivyo nyota zao zinavyoonesha jinsi gani zilivyo karibu. ATAJA ASILI… “Mwenye nyota ya ng’e asili yake ni maji na nyota ya mizani asili yake ni hewa...

HOTUBA YA MHE MCHUNGAJI PETER SIMON MSIGWA, AKITANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, TAREHE 14 MWEZI JUNI, 2020, MJINI DODOMA

“ Nataka kuwa Rais wa Ndoto Yako.” I. UTANGULIZI Waheshimiwa Wananchi Wenzangu wa Tanzania na marafiki wa nchi yetu; Tarehe 25 Mwezi Oktoba Mwaka huu (2020) tunakwenda kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani wa kuiongoza nchi yetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Kwa kawaida, uchaguzi ni kipindi kinachompa kila mwananchi fursa na wajibu wa kuhakikisha tunapata sera na uongozi bora, kwa ama kujitokeza kuwania nafasi ya uongozi au kupiga kura ya kumchagua mtu sahihi wa kuliongoza vema Taifa letu. Ndugu Wananchi, kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Mimi Mchungaji Peter Simon Msigwa, nimeamua kuchukua wajibu wa kujitokeza ili kuipa nchi yetu fursa pana zaidi ya kupata Rais bora ambaye hajawahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Kama nilivyokwisha dokeza siku chache zilizopita, leo natangaza rasmi nia yangu ya kuwania nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na tayari, kwa mujibu wa Katiba na taratibu za chama chetu – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) - nimew...