Skip to main content

Serikali imewapongeza wasanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Salehe 'Ali Kiba.


Serikali imewapongeza wasanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Salehe 'Ali Kiba' kwa kuitangaza na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi.
Hayo yalielezwa jana bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harisson Mwakyembe wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2020-2021.
Waziri Mwakyembe alisema kwa kuzingatia ubunifu uliotukuka, wasanii wa Tanzania wameweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ikiwa ni pamoja na kuitangaza nchi.
Aliwataja wasanii wengine walioitangaza vyema nchi kuwa ni Rajabu Abdul Kahali ‘Harmonize’, Vanessa Mdee, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Sharif Thabeet ‘Darassa’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na wengine wengi.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana wasanii hawa na kuwaasa wengine kuongeza kasi na ubunifu katika kazi zao ili zivutie masoko ya ndani na nje ya nchi,” alisema Mwakyembe.
Aliongeza kuwa Baraza la Sanaa ya Taifa (BASATA) limetoa jumla ya vibali 1,620 kwa wasanii wa Tanzania kwenda nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa hadi Machi, 2020.
Pia katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 vibali vilivyotolewa na BASATA kwa muktadha huo ni 135.
Vilevile, Baraza limetoa jumla ya vibali 527 kwa wadau kuingiza wasanii wa nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa nchini ili kujifunza sanaa ya Tanzania ambapo vibali 25 vimetolewa katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi, 2020.
Pia Baraza kwa kushirikiana na ubalozi wa India nchini, lilipeleka kikundi cha sanaa cha Lumumba Theatre Group kushiriki katika Tamasha la 34 la Kimataifa la kazi za Sanaa lililofanyika Surajkund nchini India.

Comments

Popular posts from this blog

UMUHIMU WA KUFANYA SERVICE OIL KWENYE GARI LAKO

  Kufanya **ervice oil* kwenye gari ni muhimu sana kwa utunzaji na ufanisi wa injini. Hapa kuna sababu kuu za kufanya huduma hii mara kwa mara:    1.Kulinda na Kudumisha Injini - Mafuta ya injini husaidia kulainisha sehemu za injini ili zisichakazane haraka kutokana na msuguano.   - Huondoa uchafu na masalia yanayoweza kuzuia utendaji mzuri wa injini.   2. Kuboresha Utendaji wa Gari - Injini inayopata huduma ya mara kwa mara hufanya kazi kwa ufanisi zaidi.   - Inapunguza msuguano wa sehemu za ndani ya injini, hivyo kuongeza nguvu na utendaji wake.   3.Kuongeza Uhai wa Injini - Mafuta machafu yanaweza kusababisha uchakavu wa injini haraka.   - Kubadilisha mafuta mara kwa mara husaidia injini kudumu kwa muda mrefu bila matatizo makubwa.   4.Kupunguza Matumizi ya Mafuta (Fuel Consumption) - Injini safi na yenye mafuta mazuri hufanya kazi vizuri bila kutumia mafuta mengi.   - Mafuta mabovu au machafu y...

Mariah Carey Apata Pigo Kubwa: Mama na Dada Yake Wafariki Katika Siku Moja

 Mariah Carey ni mmoja wa wasanii wenye vipaji vya kipekee na wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki duniani. Amejulikana kwa sauti yake yenye upana wa oktava tano, uwezo wa kutumia miondoko ya melisma, na matumizi ya kipekee ya "whistle register". Katika mwaka wa 2023, aliorodheshwa kama msanii wa tano bora wa wakati wote na jarida la Rolling Stone. citeturn0search12 Maisha ya Awali na Mwanzo wa Muziki Mariah alizaliwa tarehe 27 Machi 1969 huko Huntington, New York. Alikuwa mtoto wa tatu wa Alfred Roy Carey, mhandisi mwenye asili ya Kiafrika na Kivenezuela, na Patricia Hickey, mwalimu wa muziki na mwimbaji wa opera mwenye asili ya Kiayalandi. Baada ya wazazi wake kutalikiana mwaka 1973, Mariah alikulia na mama yake, ambaye aligundua kipaji chake cha muziki akiwa na umri mdogo. Alianza kuandika nyimbo na kufanya maonyesho akiwa shule ya upili, na baada ya kuhitimu, alihamia Manhattan kufuata ndoto yake ya muziki. citeturn0search15 Mafanikio yake yalianza alipo...

S2Kizzy: Kutoka Mbeya Mpaka Pluto Republic – Safari ya Mfalme wa Beats za Bongo

  Maisha ya S2Kizzy: Safari ya Mtayarishaji Bora wa Muziki Tanzania Salmin Kasimu Maengo, anayejulikana zaidi kwa jina la kisanii S2Kizzy au Zombie, alizaliwa tarehe 9 Mei 1996 huko Mbeya, Tanzania. Baada ya mama yake kufariki akiwa na umri wa miaka mitatu, alilelewa na shangazi yake. Baba yake aliondoka na kuoa tena, hali iliyomfanya S2Kizzy kukua katika mazingira ya changamoto. Alianza kujifunza muziki akiwa mdogo, akicheza ngoma shuleni. Wakati wa masomo yake katika shule ya sekondari ya bweni ya Kwiro Boys High School huko Morogoro, alijifunza kutengeneza muziki kwa kutumia kompyuta ya mwalimu wake. Alitumia likizo zake kubaki shuleni, akidai kuwa alikuwa amepewa adhabu, ili aweze kuendelea na mafunzo yake ya muziki. Kipaji na Mafanikio S2Kizzy alijizolea umaarufu mkubwa kwa kutayarisha nyimbo maarufu kama "Tetema" na "Amaboko" za Rayvanny akimshirikisha Diamond Platnumz. Amefanya kazi na wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz, Rayvanny, Vanessa Mdee, Bill Nass, ...