BAADA YA KUSITISHA IBADA, ASKOFU BAGONZA AFUNGUKA ZAIDI
Uongozi wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe linaloongozwa na Askofu Dr. Benson Bagonza limesitisha ibada kwa muda hadi tarehe 31 mwezi ujao kama sehemu ya kushiriki vita dhidi ya virusi vya Corona.
Media imezungumza naye kufahamu mbali na hatua hiyo wamejiwekea mikakati gani zaidi ya kuwaeleimisha waumini ili waendelee kujikinga nje ya mikusanyiko ya ibada.
KANISA NA CORONA
Kanisa halikuitwa kwa ajili ya mambo mepesi.
1. Lilipopingwa na kuteswa, lilikimbilia pangoni (Catacomb)
2. Wakati wa Ukomunisti, lilikimbilia nyumbani
3. Lilipopigwa marufuku kisheria, lilikimbilia mioyoni
4. Lilipochomwa moto na waumini wake kuwindwa kwa upanga, liliishi magotini mafichoni na hadharani.
5. Vifungo, mashimo ya wanyama wakali, matanuru ya moto, uzushi, na ukengeufu, havikuliweza.
6. Utandawazi uliotangaza kifo cha Mungu, haujaliweza.
7. Hata Virusi vya Corona, havitaliweza.
Kukosekana kwa Usahihi wa maamuzi au upungufu wa tafakuri si zuio la kuchukua hatua za kunusuru uhai. Tunaweza kuwa tumechelewa, lakini tumefanya.
Kanisa la kweli linaanzia nyumbani.
This is the best time to be the church. Beyond the four walls, we are stronger.
Comments
Post a Comment