Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

SIWEZI KUFANYA COLLABORATION NA WA BONGO

SIWEZI KUFANYA COLLABORATION NA WA BONGO. Msanii maarufu hapa Africa Davido Amesema hajaona mwanamziki kutoka Bongo anayeweza kufanyanae Collabo na ikawa hit Song. Alipoulizwa Kuhusu Diamond Platnumz na Alikiba, Davido akasema hawezi Kufanya Collabo na wasanii hao kwani anajua wasanii hao wapo Level ya chini Sana. LIKE COMMENT SHARE  KWENYE MAGROUP USISAHAU KULIKE PAGE HII SASA NI

Serikali imewapongeza wasanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Salehe 'Ali Kiba.

Serikali imewapongeza wasanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Salehe 'Ali Kiba' kwa kuitangaza na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi. Hayo yalielezwa jana bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harisson Mwakyembe wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2020-2021. Waziri Mwakyembe alisema kwa kuzingatia ubunifu uliotukuka, wasanii wa Tanzania wameweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ikiwa ni pamoja na kuitangaza nchi. Aliwataja wasanii wengine walioitangaza vyema nchi kuwa ni Rajabu Abdul Kahali ‘Harmonize’, Vanessa Mdee, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Sharif Thabeet ‘Darassa’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na wengine wengi. “Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana wasanii hawa na kuwaasa wengine kuongeza kasi na ubunifu katika kazi zao ili zivutie masoko ya ndani na nje ya nchi,” alisema Mwakyembe. Aliongeza kuwa Baraza la Sanaa ya Taifa (BASATA) limetoa jumla ya vibali 1,620 kwa wasanii wa Tanz...

WHO ILIJUA VIRUSI VYA CORONA MIAKA MIWILI ILIYO PITA

WHO ilijua kuhusu virusi vya corona miaka miwili iliopita. Mnamo mwezi Februari 2018, kundi la wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO) lilichapisha orodha ya magonjwa ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele katika uangalizi na utafiti kutokana na tishio kubwa yanayotoa. Orodha ya magonjwa manane ilishirikisha Ebola, Zika, Homa ya Lasa, Homa ya Rift Valley, Homa ya Crimean Congo, Ugonjwa wa Nipha na magonjwa ya mapafu ya SARS na MERS. Lakini ugonjwa mmoja zaidi ulikuwepo na ukapewa jina X. Ugonjwa huo WHO ilisema kwamba utatoa mlipuko hatari wa kimataifa na utasababishwa na viini vinavyoweza kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu. ''Kweli Covid 19 ndio ugonjwa uliopewa jina X'', alisema Dkt. Josie Golding, Mkuu wa Magonjwa ya Milipuko katika shirika la kufanya tafiti mjini London.
CORONA: MAITI ZA WAAFRIKA ZITATAPAKAA MITAANI – MELINDA GATES MELINDA GATES, mke wa bilionea Bill Gates wa Marekani, ameonya kwamba iwapo dunia na hususani Afrika haitachukua hatua za haraka za kukabiliana na janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, maiti za Waafrika zitatapakaa katika kila mitaa ya Afrika mijini na Vijijini. Bi Gates ametoa onyo hilo akizungumza na shirika la habari CNN la Marekani, kuhusu athari kubwa itakayozikumba nchi masikini duniani hususani Afrika. Alisema moyo wake uko Afrika na kwamba ana wasiwasi mkubwa kwamba bara hilo huenda likashindwa kukabili madhara makubwa ya virusi hivyo. “Litakuwa janga la kutisha katika nchi zinazoendelea. Baadhi ya sababu zinazoonyesha kwamba idadi haijafikia hali mbaya Afrika, ni kwa kuwa watu wengi hawapimwi kutokana na Afrika kukabiliwa na uhaba wa vifaa vya kupima na hata pale watu wanapopimwa mamlaka za Afrika zimekuwa zikificha baadhi ya taarifa na kuripoti takwimu za visa vya Corona chini ya ki...
BAADA YA KUSITISHA IBADA, ASKOFU BAGONZA AFUNGUKA ZAIDI Uongozi wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe linaloongozwa na Askofu Dr. Benson Bagonza limesitisha ibada kwa muda hadi tarehe 31 mwezi ujao kama sehemu ya kushiriki vita dhidi ya virusi vya Corona. Media imezungumza naye kufahamu mbali na hatua hiyo wamejiwekea mikakati gani zaidi ya kuwaeleimisha waumini ili waendelee kujikinga nje ya mikusanyiko ya ibada. KANISA NA CORONA Kanisa halikuitwa kwa ajili ya mambo mepesi. 1. Lilipopingwa na kuteswa, lilikimbilia pangoni (Catacomb) 2. Wakati wa Ukomunisti, lilikimbilia nyumbani 3. Lilipopigwa marufuku kisheria, lilikimbilia mioyoni 4. Lilipochomwa moto na waumini wake kuwindwa kwa upanga, liliishi magotini mafichoni na hadharani. 5. Vifungo, mashimo ya wanyama wakali, matanuru ya moto, uzushi, na ukengeufu, havikuliweza. 6. Utandawazi uliotangaza kifo cha Mungu, haujaliweza. 7. Hata Virusi vya Corona, havitaliweza. Kukosekana kwa Usahihi wa maamuzi au upungufu wa taf...
Msanii wa bongo fleva, Elias Barnaba maarufu Barnaba amesema mpango wake aliokuwa nao kwa sasa ni kufuta tattoo ya mama mtoto wake anayeitwa Zuu Namella ambayo ameichoro mkononi mwake. Akiiambia WasafiTv, Barnaba alisema kama mtu akiachana na mpenzi wake hana haja ya kubaki na alama yoyote kwasababu inamkubushia machungu. Alisema alijitahidi kuvumilia lakini anaona machungu yanaongezeka hivyo anahitaji kuifuta ili kuwa sawa. “Nimepitia maumivu na machungu mengi hivyo sihitaji kubaki na alama ya mtu ambayo nimempoteza hivyo ninampango wa kuifuta ili kumsahau kabisa". Itakumbukwa, Barnaba na Zuu walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume na kumpa jina la # Steve . Mama Steve amefunga ndoa wikiendi iliyomalizika na mpenzi wake.

Covid 19

Tazama vitu ambavyo vina pelekea kuleta mahambukizi Nakuenea kwa coro corona vairas covid 19 #Staysafe #Stayhome corona vairas ni hatari