TAIFA STARS YA SHINDA UGENINI DHIDI YA MPIZANI WAKE GUINEA
Taifa Stars, timu ya taifa ya Tanzania, ilicheza mechi muhimu ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Guinea tarehe 10 Septemba 2024. Katika mechi hiyo, Taifa Stars walipambana vikali dhidi ya Guinea na kupata ushindi wa mabao 2-1. Mchezo huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Charles Konan Banny, Cote d'Ivoire, na ulikuwa sehemu ya kampeni ya kufuzu AFCON 2025.
Kabla ya mechi hiyo, Taifa Stars walikuwa wametoka sare ya 0-0 dhidi ya Ethiopia katika mchezo wao wa kwanza wa kundi H, hali iliyosababisha mashabiki wengi kutokuwa na matumaini makubwa kutokana na mbinu zao za kujihami nyumbani. Kocha wa Taifa Stars, Hemed "Morocco" Suleiman, alisisitiza kuwa timu ilikuwa imejipanga vyema kwa mchezo dhidi ya Guinea, akibainisha kuwa walikuwa wamefanya marekebisho kadhaa baada ya sare hiyo ya awali.
Comments
Post a Comment