Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2020

HOTUBA YA MHE MCHUNGAJI PETER SIMON MSIGWA, AKITANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, TAREHE 14 MWEZI JUNI, 2020, MJINI DODOMA

“ Nataka kuwa Rais wa Ndoto Yako.” I. UTANGULIZI Waheshimiwa Wananchi Wenzangu wa Tanzania na marafiki wa nchi yetu; Tarehe 25 Mwezi Oktoba Mwaka huu (2020) tunakwenda kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani wa kuiongoza nchi yetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Kwa kawaida, uchaguzi ni kipindi kinachompa kila mwananchi fursa na wajibu wa kuhakikisha tunapata sera na uongozi bora, kwa ama kujitokeza kuwania nafasi ya uongozi au kupiga kura ya kumchagua mtu sahihi wa kuliongoza vema Taifa letu. Ndugu Wananchi, kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Mimi Mchungaji Peter Simon Msigwa, nimeamua kuchukua wajibu wa kujitokeza ili kuipa nchi yetu fursa pana zaidi ya kupata Rais bora ambaye hajawahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Kama nilivyokwisha dokeza siku chache zilizopita, leo natangaza rasmi nia yangu ya kuwania nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na tayari, kwa mujibu wa Katiba na taratibu za chama chetu – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) - nimew...