Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2020

JACQUELINE WOLPER SINA TABIA YA KURUDIANA WALA KUONGEA NA EX

SINA TABIA YA KURUDIANA WALA KUONGEA NA EX Msanii wa filamu Jacqueline Wolper amepiga stori kwenye show ya Dadaz ya East Africa TV na kufunguka mambo mengi ikiwemo mahusiano yake, biashara na kuhama jiji la Dar es Salaam na kuhamia Arusha. Kuhusu ishu za mahusiano yake msanii huyo amesema, kwanza hana tabia ya kuongea wala kurudiana na Ex wake na kwa sasa ana wanaume wanne na atachagua mmoja wa kuwa naye. "Nina wapenzi kama wanne kwa sasa ila naangalia na kuchagua mmoja mwenye tabia njema ndiyo nitakuwa naye, ila nipo nao kwa njia ya mawasiliano sio kufanya mapenzi pia sijafanya mapenzi kwa miaka minne sasa nimetulia tu, maana kila siku watu wananipa mabwana wapya" amesema Wolper . "Sinaga tabia ya kurudiana wala kuongea na Ex wangu, na sijawahi kupenda mume wa mtu maana mimi nina wivu na napeda uhuru wa kuwa na mwanaume wangu, siku ambayo nitakuja kumpost Instagram labda awe amenipa mimba au amenioa" ameongeza Nini maoni yako